Wanamgambo wa Mai Mai katika Jamhuri
ya Kidemokrasia ya Kongo wametoa wito wa kujumuishwa katika mazungumzo
ya amani baina ya serikali na waasi wa M23. Joseph Assanda mmoja wa
viongozi wa wanamgambo wa Mai Mai katika Jimbo la Kivu Kusini amesema
kuwa, kundi lao linapaswa kujumuishwa katika mazungumzo ya amani baina
ya serikali na M23. Hayo yanajiri katika hali ambayo, mazungumzo ya
waasi wa M23 na serikali ya Kinshasa yaliyokuwa yakifanyika mjini
Kampala Uganda, yameendelea kukosolewa na wapinzani ambao wanataka
makundi mengine ya upinzani yajumuishwe katika mazungumzo hayo. Wakati
huo huo,
mazungumzo ya amani kati ya serikali ya Kinshasa na waasi hao
yanatarajiwa kuendelea tena mwezi huu wa Januari baada ya kumalizika
sherehe za Krismasi na mwaka mpya. Tangu Mei mwaka jana zaidi ya watu
laki tisa wamelazimika kuyakimbia makazi yao mashariki mwa Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Kongo kufuatia machafuko na ukosefu wa usalama katika
maeneo hayo. Baadhi ya raia hao wamelazimika kukimbilia katika nchi
jirani za Rwanda na Uganda.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment