Social Icons

rss feed facebook twitter google plus linkedin youtube email

Wednesday, January 9, 2013

Sakata ya Polisi Feki Kenya yalitikisa jeshi la polisi


Sakata ya Polisi Feki Kenya yalitikisa jeshi la polisi
Sakata ya kuweko afisa bandia wa polisi, Joshua Karianjahi Waiganjo aliyehudumu kwa takriban miaka mitano kama afisa wa ngazi za juu mkoani Rift Valley katika jeshila polisi huko nchini Kenya imeendelea kuwaandama wakuu wa polisi katika mikoa kadhaa ya nchi hiyo. Hapo jana Inspekta Mkuu wa Polisi David Kimaiyo aliwafuta kazi maafisa kadhaa wa ngazi za juu katika jeshi la polisi akiwemo Mkuu wa polisi katika mkoa wa Rift Valley, John Mbijiwe. Shoka hilo pia limemuangukia afisa mkuu wa kitengo cha kupambana na wizi wa mifugo Remi Ngungi. Imedaiwa kuwa,
Wanjohi alikuwa na uwezo mkubwa na kwamba aliwahi hata kuwafuta kazi maafisa kadhaa wa polisi na uamuzi wake kuidhinishwa na wakuu wa polisi. Siku kadhaa zilizopita, Rais Mwai Kibaki aliagiza kuundwa mara moja kamati ya kuchunguza sakata hiyo ambalo limeiletea aibu kubwa jeshi la polisi na serikali kwa ujumla.

No comments:

Post a Comment