Serikali ya Eritrea imesema kuwa, hali katika mji mkuu
Asmara ni tulivu baada ya kushindwa nguvu wanajeshi waasi waliokuwa
wamechukua udhibiti wa jengo la Wizara ya Habari.
Yemane Gebremeskel, mkurugenzi wa ofisi ya Rais Issaias Afeworki wa Eritrea amethibitisha kutulia hali ya mambo.
Kundi moja la askari waasi katika Jeshi la Eritrea
walizingira Wizara ya Habari Jumatatu na kulazimisha Shirika la
Utangazaji la Taifa kutangaza kuachiliwa huru wafungwa wote wa kisiasa.
Wanajeshi hao waasi walimlazimisha mkuu wa televisheni ya serikali kusoma tangazo hilo.
Kwa kawaida huwa vigumu kuthibitisha habari kutoka Eritrea kwani hakuna chombo chochote cha habari cha kigeni nchini humo.
Duru za wapinzani zinasema kuwa, wanajeshi hao waasi
wapatao 100 walisalimu amri baada ya serikali kusema itatelekeza matakwa
yao. Mwaka jana Umoja wa Mataifa ulikadiria kuwa, kuna kati ya wafunwa
elfu tano hadi elfu kumi wa kisiasa nchini Eritrea.
No comments:
Post a Comment