Social Icons

rss feed facebook twitter google plus linkedin youtube email

Thursday, January 3, 2013

Waislamu washambuliwa na kuteswa Marekani


Waislamu washambuliwa na kuteswa  MarekaniVitendo vya ukandamizaji, utesaji na ushambuliaji dhidi ya Waislamu vimeongezeka kwa kasi kubwa nchini Marekani. Televisheni ya Russia Today imeinukuu Polisi ya Marekani FBI ikisema kuwa, mashambulizi yanayosababishwa na chuki dhidi ya Waislamu nchini Marekani yaliongezeka kwa asilimia 50 mwaka 2010. Maisha ya Waislamu yamekuwa hatarini zaidi nchini humo tokea lilipotokea shambulio la Septemba 11, na Waislamu wa Marekani na wahajiri walioko nchini humo wamekuwa wakikabiliwa na vitendo vya kibaguzi, ukandamizaji, utesaji na wengine kupigwa bila ya hatia yoyote,
huku baadhi ya vyombo vya kupasha habari na hata taasisi na asasi za kiserikali za Marekani zikishajiisha vitendo  hivyo vilivyo dhidi ya ubinadamu. Nadhira al Khalili Wakili na Mshauri wa Masuala ya Kisheria wa Baraza la Uhusiano wa Marekani na Uislamu amesema kuwa, kanali za televisheni kama vile Fox News mara nyingi huwaarifisha Waislamu kuwa magaidi, na kuwapotosha watu walio na uelewa mdogo. Wakili Nadhira ameongeza kuwa, baadhi ya washambuliaji wamekiri kwenye vituo vya polisi kuwa wamewashambulia Masingasinga na Wahindu wakidhani kwamba ni Waislamu. Al Khalili ameongeza kuwa, Waislamu mithili ya watu wengine ni watu wenye kupenda amani na utulivu nchini humo.

No comments:

Post a Comment