Social Icons

rss feed facebook twitter google plus linkedin youtube email

Wednesday, January 9, 2013

Shughuli za kukusanya maoni ya katiba TZ zachafuka


Shughuli za kukusanya maoni ya katiba TZ zachafukaMwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba nchini Tanzania amejikuta mashakani baada ya kutoa agizo la kupinga kutolewa baadhi ya maoni na wananchi. Jaji Mustaafu Joseph Warioba anayeongoza tume hiyo yenye dhima ya kukusanya maoni kuhusu katiba mpya ameagiza maafisa kutopokea maoni ya makundi maalumu. Warioba amesema watu watoe maoni yao binafsi bila kufungamana na makundi yoyote. Hatua hiyo imemuweka pabaya jaji huyo mustaafu baada ya makundi ya kutetea haki za binadamu kusema kuwa, agizo hilo ni ukiukaji wa haki ya kujieleza.
Huku hayo yakijiri watumishi wa umma wamepata fursa ya kutoa maoni yao kuhusu katiba mpya. Miongoni mwa mambo yaliyotawala kikao chao na maafisa wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba ni suala la mishahara bora pamoja na kuboreshwa mazingira yao ya kazi. Tume hiyo inatarajiwa kumaliza kazi zake mwezi Mei mwaka huu na kisha kura ya maoni kuitishwa baadaye.
Na: Salim Swaleh

No comments:

Post a Comment