Social Icons

rss feed facebook twitter google plus linkedin youtube email

Wednesday, January 9, 2013

Waasi wa Seleka wazungumza na wakuu wa CAR


Waasi wa Seleka wazungumza na wakuu wa CAR
Mazungumzo kati ya muungano wa waasi wa Seleka na wawakilishi wa serikali ya Jamhuri ya Afrika ya Kati yameanza leo huko Libreville mji mkuu wa Gabon. Mazungumzo hayo yanafanyika chini ya upatanishi wa nchi za eneo la katikati mwa bara la Afrika. Imeelezwa kuwa, ajenda kuu ya mazungumzo hayo ni kujadili kwa kina makubaliano yaliyofikiwa hapo awali kati ya pande hizo mbili katika miaka ya 2007 na 2011. Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Jamhuri ya Congo Brazzaville Basile Ikouébé ambaye ni Mwenyekiti wa mazungumzo hayo amezitaka pande mbili kuheshimu sheria za Umoja wa Afrika zinazopiga marufuku kuondoshwa kiholela tawala zilizopo madarakani.

Muungano wa waasi wa Seleka tarehe 10 mwezi uliopita ulianzisha harakati za kijeshi dhidi ya serikali ya Rais Francois Bozize wa Jamhuri ya Afrika ya Kati, ukilalamikia kupuuzwa vipengee vya makubaliano ya pande mbili. Waasi hao walifanikiwa kudhibiti miji kadhaa ya nchi hiyo sanjari na kumtaka Rais Bozize ang'atuke madarakani. Kuingia kwa vikosi vya kimataifa huko Jamhuri ya Afrika ya Kati kumewazuia waasi hao kusonga mbele kuelekea Bangui, mji mkuu wa nchi hiyo.

No comments:

Post a Comment