Rais wa eneo la Puntland lenye
mamlaka ya ndani kaskazini mashariki mwa Somalia amejiongezea muda wa
kutawala hadi Januari mwaka ujao wa 2014.
Akizungumza mjini Bodsaso, Rais
Abdulrahman Mohammad Farole wa Puntland amesema ataendelea kutawala
baada ya muhula wake kumalizika mwezi huu.
Farole amesema katiba inamruhusu kuongeza muhula wake kwa muda wa mwaka mmoja.
Wapinzani wanamlaumu rais huyo wa Puntland kuwa amekiuka sheria.
Eneo la Puntland lilijitangazia mamlaka
ya ndani mwaka 1998 na limekuwa likishuhudia amani pamoja na kuwepo vita
katika maeneo ya kati na kusini mwa Somalia.
Eneo la Somaliland lililoko kaskazini
mwa Somalia tayari limeshajitangazia uhuru kamili ingawa bado
halijatambuliwa na Umoja wa Mataifa.
No comments:
Post a Comment