Duru za habari kutoka nchini Iraq
zimearifu kuwa, zaidi ya watu 25 wameripotiwa kuuawa katika maeneo
tofauti nchini humo. Habari zinasema kuwa, mauaji hayo yalitokea jana
katika mfululizo wa miripuko ya mabomu iliyotokea katika maeneo tofauti
nchini Iraq. Mauaji hayo yanajiri baada ya mfululizo wa mauaji
yaliyosababishwa na mashambulizi ya kigaidi yaliyotokea katika siku tatu
zilizopita kwenye maeneo kadhaa ya nchi hiyo, na kupelekea kuuawa zaidi
ya watu 81 na kujeruhiwa mamia ya wengine. Hadi sasa hakuna kundi
lolote lililotangaza kuhusika na mauaji hayo. Viongozi wa Iraq wamekuwa
wakizituhumu nchi za Saudia na Qatar kuwa, zinayaunga mkono makundi ya
kigaidi yanayofanya mauaji nchini humo, kama njia ya kutekeleza siasa za
Marekani kwenye eneo la Mashariki ya Kati. Wakati huo huo serikali ya
Baghdad imetangaza kuwa, polisi ya nchi hiyo imefanikiwa kuwaangamiza
magaidi 10 katika mkoa wa Al-Anbar nchini humo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment