Wanajeshi wa Mali wamepambana vikali
na wanamgambo wanaokalia eneo la kaskazini katika mji wa Konna ulioko
katika eneo la katikati mwa nchi hiyo.
Wakaazi wa Konna wanasema siku ya
Jumatano kulikuwa na ufyatulianaji risasi wa masaa kadhaa kati ya waasi
na wanajeshi wa serikali.
Mapigano hayo yamejiri masaa 48 baada ya vikosi vya serikali kujaribu kuudhibti mji huo.
Duru mpya ya mashambulizi ya waasi
inajiri baada ya mazungumzo ya amani kati ya pande hasimu kuakhirishwa.
Mazungumzo hayo yalikuwa yaanze leo katika mji mkuu wa Burkina Faso,
Ouagadougou.
Kabla ya hapo kulitangazwa kuwepo
maandalizi ya waasi wanaofungamana na kundi la Ansarud-Din na Harakati
ya Umoja na Jihad katika eneo la Magharibi mwa Afrika, kwa ajili ya
kufanya mazungumzo na serikali ya Bamako ili kuupatia ufumbuzi mgogoro
unaoendelea kutokota nchini humo.
No comments:
Post a Comment