Hayo yamedokezwa na Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa huko Somalia, Balozi Augustine Mahiga.
Balozi Mahiga amesema kuwa wakimbizi hao wa Somalia wanarejea katika nchi yao kwa hiari yao wenyewe kutokana na kuimarika kwa hali ya usalama.
Hata hivyo Balozi Mahiga amesema kuwa, kurejea wakimbizi hao ni changamoto kwa serikali ya Somalia kwa sababu haijajiandaa ipasavyo.
Ameongeza kuwa Jumuiya ya Kimataifa inapaswa kusaidia serikali ya Somalia kuhakikisha inasaidia wakimbizi hao kurejea katika maisha ya kawaida ndani ya nchi yao.
Wakati huo huo Mwakilishi Maalumu wa Mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika nchini Somalia, Balozi Mahamat Annadif amesema umoja huo utaendelea kuunga mkono juhudi za amani Somalia.
Ameongeza kuwa vikosi vya Umoja wa Afrika Somalia AMISOM vitaendelea kushirikiana na taasisi za usalama nchini humo ili kuhakikisha amani inarejea kikamilifu katika nchi hiyo ya Pembe ya Afrika
No comments:
Post a Comment