Mshukiwa wa mauaji ya kimbari nchini
Rwanda Leon Mugesera amefungua kesi akitaka majaji wawili kati ya
watatu wanaosikiliza kesi yake waondolewe.
Mugesera alifikishwa kizimbani katika
Mahakama Kuu ya Rwanda lakini punde baada ya kuwasili hapo alifungua
kesi akitaka majaji Athanase Bakuzakundi na Eugene Ndagijimana wazuiwe
kusikiliza kesi yake. Amesema kwa mujibu wa sheria ya taratibu za
mahakama, majaji hao hawana haki ya kusikiliza kesi yake kwani waliwahi
kusikiliza kesi zake ambazo alishindwa.
Mahakama inatazamiwa kutoa uamuzi wake
leo Alkhamisi kuhusu pingamizi hiyo ya Mugesera ambaye alirejeshwa
Rwanda kutoka katika maficho yake nchini Canada.
Mugesera anakabiliwa na mashtaka ya kushiriki katika mauaji ya kimbari ya mwaka 1994 nchini Rwanda.
No comments:
Post a Comment