Friday, February 1, 2013
Shahidi adai kina Ponda walivamia eneo
(TANGAZO LA KONGOMANO La Waislamu Jumapili ya Februari 3.)
MLINZI wa Kampuni ya Agritanza Ltd, Julius Mlanzi ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jinsi kundi la Waislamu lilivyofika na kutaka warejeshewe eneo La Makazi lililopo Chang’ombe, mali ya waislamu.
Mlinzi huyu Alidai mahakamani kuwa Waislamu hao Wamemtaka mmiliki wa eneo hilo kuwasiliana na aliyemuuzia ili arejeshewe fedha alizotoa kwa madai wao wamefika kuchukua mali yao.
Katika kesi hiyo, Sheikh Ponda issa Ponda, na, Shekhe Mukadam Abdallah Swalehe na waislamu wengine 48 wanakabiliwa na mashtaka manne, likiwamo la uchochezi na wizi wa mali yenye thamani ya Sh59.6 milioni.
alidai shahidi huyo. Shahidi wa sita wa upande wa mashtaka, Hamis Mkangama, akitoa ushahidi wake mahakamani hapo alidai kuwa Oktoba 7, mwaka jana akiwa katika eneo hilo la Chang’ombe Malkazi, Shekhe Ponda akiwa na mwenzake walikwenda katika eneo hilo na kupiga picha za eneo hilo.
Mkangama alidai kuwa kabla ya Sheikh huyo kuchukua picha za eneo hilo, aliwaambia nani aliwaruhusu kujenga katika eneo hilo, na kwamba wakamjibu kuwa aliwaambia wajenge ni bosi wao Suleiman.
Shahidi huyo alidai kuwa baada ya kumwambia hivyo, Sheikh Ponda aliwaambia wasimamishe ujenzi wa uzio na wao wakamweleza kuwa hawawezi kusimama hadi bosi wao aliyewaambia wajenge awaeleze hivyo.
Baada ya kumaliza kutoa ushahidi huo, Hakimu Nongwa aliiahirisha kesi hiyo hadi Februari 14, mwaka huu itakapotajwa na kwamba itaendelea kusikilizwa Februari 18, 25,27 na 28, mwaka huu.
Wakati kesi hiyo ilipokuwa ikiendelea na ilipomalizika askari wa Jeshi la Polisi na Magereza waliimarisha ulinzi katika eneo lote la mahakama kana kwamba wako Vitani.
Ilipofika saa 5:08 asubuhi msafara wa kumpeleka Sheikh Ponda gerezani ulianza ambapo kulikuwapo na magari sita aina ya ‘Defender’ yaliyokuwa yamebeba askari waliovalia mavazi maalumu na silaha kali.
Pia lilikuwapo gari la maji ya kuwasha na basi moja la Magereza lililokuwa limembeba Sheikh Ponda Issa Ponda na Waislamu wenzake.
Hata hivyo wakati msafara huo, ukitoka katika eneo la mahakama Baadhi ya Waislamu waliokusanyika katika eneo hilo walijipanga na kuanza kusema TAKBIIR ALLAHU AKBAR huku wakimuaga Shekhe Ponda Issa Ponda na waislamu wengine waliopamoja naye‘ naye sheikh alikuwa akiinua mikono yake juu iliyokuwa imefungwa pingu kama ishara ya kuwaunga mkono.
Waislamu hao wakati wakiendelea na tukio hilo, wengine walikuwa wakisambaziana vikaratasi vilivyokuwa na ujumbe ulioandikwa kuwa Bismilahir Rahmaanir Rahiimi, Kongamano, Kongamano, Kongamano.
Jumuiya ya Taasisi za Kiislamu pamoja na Shura ya Maimamu (T), Waislamu wote Jumapili ya Februari 3, mwaka huu kuanzia saa 4:00 mchana Waislamu wote wakutane katika Kiwanja cha Nuurul Yaqiin ( Uwanja wa Pamba) karibu na Uwanja wa Mwembe Yanga.
Masheikh wetu wananyimwa hata haki ya dhamana, wanazidi kuteseka jela! Sababu ni kutetea mali za Waislamu zinazozidi kuuzwa na kuporwa! Tujumuike sote pamoja katika kuonyesha mshikamano wetu na tutoe uamuzi wa pamoja nini cha kufanya, Haki lazima itendeke kwa sote kama Jamii ya Watanzania. Muislamu wa kweli hatakubali kudhulumu wala kudhulumiwa.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment