Jamhuri
ya Kiislamu ya Iran imeonyesha ndege yake ya kivita iliyotengenezwa
hapa nchini ambayo uwezo wake ni sawa na ndege ya kivita ya Marekani ya
F/A 18. Ndege hiyo ya kivita yenye jina la Qaher-313 yaani mshindi
imeonyeshwa katika marasimu yaliyofanyika leo Jumamosi na kuhudhuriwa na
Meja Jenerali Ataollah Salehi Kamanda wa Jeshi la Iran, Waziri wa
Ulinzi wa Iran Brigedia Jenerali Ahmad Vahidi na Kamanda wa Jeshi la
Anga la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Brigedia Jenerali Hassan Shah Safi
katika maadhimisho ya Alfajiri Kumi katika kukumbuka ushindi wa
Mapinduzi ya Kiislamu mwaka 1979.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment