Rais Francois Hollande wa Ufaransa
amesema vikosi vya nchi hiyo vitaendelea na operesheni zake huko
kaskazini mwa Mali lakini vitakabidhi kwa wakati hatamu za uendeshaji
operesheni hizo kwa vikosi vya askari wapatao 8,000 wa nchi za Afrika.
Hollande ameyasema hayo leo alipokutana na vikosi vya Ufaransa huko
Timbuktu wakati wa safari yake ya siku moja nchini Mali huku kukiwepo
madai kwamba raia wa kawaida wameuawa kutokana na mashambulio ya anga ya
Ufaransa sambamba na mauaji ya kikabila wakati wa operesheni hiyo ya
kuingilia kijeshi huko kaskazini mwa Mali.
Kwa mujibu wa duru za habari
hadi sasa malengo mawili ya operesheni ya kijeshi ya Ufaransa huko Mali
yameshafikiwa ambayo ni kuwazuia waasi wasisonge mbele kuelekea kusini
na kuikomboa miji iliyokuwa imetekwa na waasi hao. Hata hivyo lengo kuu
la tatu kama lilivyoelezwa na Rais wa Ufaransa ambalo ni kurejesha
udhibiti wa ardhi yote ya Mali kama taifa moja na chini ya uongozi wa
serikali kuu bado halijafikiwa.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment