skip to main |
skip to sidebar
‘Sudan Kusini inapanga kuvuruga amani ya Sudan’
Chama cha Kongress ya Taifa kinachotawala nchini Sudan,
kimefichua njama iliyoratibiwa na Sudan Kusini kwa kushirikiana na
Marekani na utawala haramu wa Kizayuni, kwa ajili ya kuharibu hali ya
amani nchini humo. Chama hicho kimefafanua kuwa, Sudan Kusini kwa
kushirikiana na Marekani na utawala haramu wa Kizayuni inafanya njama ya
kuzusha machafuko katika maeneo ya Kordofan Kusini na katika jimbo la
Darfur kwa kuwaunga mkono wapinzani wa serikali ya Khartoum. Aidha chama
hicho kimesisitiza kuwa, njama hiyo ina lengo la kuandaa uwanja kwa
Marekani na utawala ghasibu wa Israel katika Baraza la Usalama la Umoja
wa Mataifa, kuituhumu Khartoum na hivyo kupelekea kuongezwa vikwazo
dhidi ya Sudan.
Qutbi Al-Mahdi mkuu wa ofisi ya Chama cha Kongress ya
Kitaifa nchini Sudan pia amesema kuwa, askari wanaoungwa mkono na Juba
wanaendelea kutekeleza ajenda za madola ya kigeni ukiwemo utawala wa
Kizayuni kwa lengo la kuvuruga usalama wa nchi hiyo.
No comments:
Post a Comment