Tanzania imepata tunzo tatu za
maajabu saba ya Afrika kupitia vivutio vyake bora vya utalii vya Mlima
Kilimanjaro, Hifadhi ya Ngorongoro na Hifadhi ya Serengeti ambavyo
viliongoza kwa kupata kura nyingi kuliko nchi nyingine yoyote.
Akitangaza matokeo hayo mjini Arusha kaskazini mwa Tanzania mbele ya
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, mkuu wa taasisi iliyoandaa tunzo hiyo Dk.
Phillip Imler wa Marekani, amesema, ushindi huo umetokana na kuwa
Tanzania ina vivutio vya kipekee. Akielezea hifadhi ya taifa ya
Serengeti, alisema kuwa ndiyo hifadhi ya kipekee iliyopata kura nyingi
kutokana na tabia ya misafara ya wanyama wanaohama kwa msimu.
Naye
Waziri Mkuu wa Tanznaia Mizengo Pinda ambaye alikuwa mgeni rasmi katika
hafla hiyo amesema kuwa nchi za Afrika zina vivutio vingi vya utalii na
fursa kubwa ya kukuza pato kupitia utalii huo. Aidha Waziri Mkuu wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ameongeza kuwa, anaamini kutokana na
sifa ambayo Tanzania imeipata kupitia vivutio vyake hivyo vitatu
itaendelea kuvitunza na kuhakikisha kuwa vinavutia zaidi watalii na
kuongeza pato la taifa.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment