Serikali ya Nigeria imesema kuwa ipo tayari kuangalia pendekezo lililotolewa na kundi la Boko Haram la kusitisha mapigano. Makamu
wa Rais wa Nigeria Namadi Sambo amesema, Abuja inakaribisha pendekezo
hilo la usitishaji mapigano la Boko Haram na kwamba serikali itajitahidi
kuhakikisha kwamba amani inapatikana nchini humo. Sambo amesema hayo
alipotembelea mji wa kusini mashariki mwa Nigeria wa Maiduguru ambao
unahesabiwa kuwa ngome ya wapiganaji wa Boko Haram. Hii ni mara ya
kwanza mji huo kutembelewa na Makamu wa Rais tangu mwaka 2009.
Kundi
lililofurutu ada la Boko Haram limehusika katika milipuko na
mashambulizi tofati katika miji kadhaa ya Nigeria tangu mwaka 2009.
Makundi ya kutetea haki za binadamu yanasema kuwa, zaidi ya watu 1000
wameuawa kutokana na mashambulizi ya kundi hilo kuanzia mwaka 2009 hadi
mwaka uliopita wa 2012.
No comments:
Post a Comment