skip to main |
skip to sidebar
Jinai za kivita za Israel dhidi ya Wapalestina
Wachunguzi wa haki za binaadamu katika Umoja wa Mataifa wameutaka
utawala wa Israel kusitisha upanuzi wa vitongoji vya waloezi wa
Kizayuni na kuwaondoa walowezi nusu milioni katika Ukingo wa Magharibi
wa Mto Jordan. Katika taarifa iliyotolewa Alkhamisi jopo la Umoja wa
Mataifa limesema hatua ya kujenga vitongoji vya walowezi wa Kizayuni
katika ardhi za Palestina ni jambo ambalo linaweza kuhesabiwa kuwa jinai
za kivita. Ripoti hiyo imeongeza kuwa ulowezi wa Wazayuni umechangia
ukiukaji wa haki za Wapalestina kwa njia nyingi.
Bi. Christine Chanet aliyeoongoza jopo hilo amesema Israel inakiuka
Mkataba wa Geneva kwa kujenga vitongoji vya walowezi wa Kizayuni katika
ardhi za Palestina. Baada ya kutolewa ripoti hiyo, Katibu Mkuu wa Umoja
wa Mataifa amesisitiza kuwa Israel inapaswa kusitisha harakati za ujenzi
wa vitongoji katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu ikiwa ni
pamoja na Quds Mashariki. Mamlaka ya Ndani ya Palestina imetishia
kuichukulia Israel hatua za kisheria katika Mahakama ya Kimataifa ya
Jinai (ICC) iwapo Tel Aviv itaendeleza ujenzi katika maeneo ya Palestina
inayoyakaliwa kwa mabavu.
No comments:
Post a Comment