Social Icons

rss feed facebook twitter google plus linkedin youtube email

Friday, February 1, 2013

Waislamu Tanzania kujadili kadhia ya Sheikh Ponda



Sheikh Ponda akifungwa pingu mahakamaniViongozi wa taasisi kadhaa za Kiislamu Tanzania wameitisha mkutano wa hadhara kwa lengo la kujadili kadhia ya Sheikh Ponda Isa Ponda anayeshikiliwa korokoroni.
Taarifa zinasema kuwa Jumuiya ya Taasisi za Kiislamu pamoja na Shura ya Maimamu Tanzania imeitisha mkutano Jumapili Februari 3 saa nne mchana. Mkutano huo umepangwa kufanyika katika Kiwanja cha Nuurul Yaqiin karibu na Uwanja wa Mwembe Yanga mjini Dar-es-Salaam
Imearifiwa kuwa mkutano huo unatazamiwa kuonyesha mshikamano wa Waislamu na Katibu wa Jumuia na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Ponda Issa ambaye anakabiliwa na kesi ya uchochezi. Walioandaa mkutano huo wanalalamika kuwa Sheikh Ponda na wenzake wamenyimwa haki ya dhamana na wanateseka jela. Kesi ya Sheikh Ponda ilisikilizwa jana Alkhamisi na inatazamiwa kuendelea Februari 18 mwezi huu.

No comments:

Post a Comment