Haki za Waislamu nchini Uingereza
zimeendelea kukiukwa huku wafungwa wa Kiislamu wanaotumikia vifungo
katika magereza ya nchi hiyo wakilazimishwa kula nyama ya nguruwe.
Shirika moja la kutetea haki za binadamu limetangaza kuwa, serikali ya
Uingereza imekuwa ikikiuka haki za wafungwa wa Kiislamu katika magereza
ya nchi hiyo. Taarifa zaidi zinasema, serikali ya Uingereza imekataa
kupeleka nyama halali kwa ajili ya wafungwa wa Kiislamu katika magereza
ya nchi hiyo na badala yake imekuwa ikiwalazimisha wafungwa hao wa
Kiislamu kula nyama ya nguruwe ambayo kwa mujibu wa mafundisho ya dini
yao ni haramu.
Imeelezwa kuwa, katika baadhi ya magereza wahusika katika
magereza hayo wamekuwa wakipeleka nyama ya nguruwe na kupuuza kwamba,
kuna wafungwa ambao ni wafuasi wa dini ya Kiislamu. Taarifa zaidi
zinaeleza kuwa, katika baadhi ya magereza nyama ya matumizi kwa ajili ya
wafungwa imepatikana ikiwa imechanganywa na nyama ya nguruwe. Shirika
linalotetea mageuzi katika magereza nchini Uingereza limetoa wito wa
kufanyika uchunguzi kuhusiana na ukiukaji wa haki za binadamu katika
magereza ya nchi hiyo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment