skip to main |
skip to sidebar
Kuna njama za kupandikiza chuki za kidini Zanzibar
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad
amesema kuwa, kuna njama za kupandikiza chuki za kidini visiwani
Zanzibar huko Tanzania. Maalim Seif ametahadharisha kuwa huenda kuna
watu wenye nia mbaya ambao wameamua kuyatumia matukio ya kuuawa na
kujeruhiwa viongozi wa kidini, kujenga chuki baada ya kuona Wazanzibari
hivi sasa ni wamoja. Maalim Seif amesema hayo alipokuwa akihutubia
katika hafla ya Maulid ya Kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (S.A.W), huko
Wilaya ya Wete, Kaskazini Pemba. Maalim Seif ambaye pia ni Katibu Mkuu
wa Chama cha Wananchi CUF amesema,
inasikitisha kuona kuwa, wapo
viongozi wenye nia chafu dhidi ya Zanzibar na wenye tabia ya kutoa kauli
za kujenga chuki na fitna miongoni mwa Wazanzibari chini ya kivuli cha
matukio hayo. Amesema, kinachoonekana kuna ajenda imetayarishwa ya
kutaka kulazimisha chuki za kidini Zanzibar, licha ya kuwa kisiwa hicho
kina historia ya dahari ya watu kuvumiliana na kuishi kwa pamoja. Makamu
wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar amewataka wananchi wote wa Zanzibar hivi
sasa wawe macho na ajenda zinazolengwa kuwavuruga, na waendelee kuishi
kwa mshikamano na umoja kama ambavyo wamekuwa wakiishi.
Na Salum Bendera
No comments:
Post a Comment