Rais Jakaya Mrisho Kikwete
wa Tanzania amesema ifikapo mwaka 2015 hakutakuwa na uhaba wa walimu
nchini humo na kwamba kuanzia mwaka 2020 shule za msingi zitaanza
kufundishwa na walimu wenye elimu ya shahada, kutokana na idadi kubwa ya
wahitimu wa fani hiyo watakaokuwa kwenye soko la ajira. Akizungumza
kwenye kongamano linalohusu masuala ya uchumi na maendeleo
lililoandaliwa na Kigoda cha Mwalimu Nyerere kwa kushirikiana na Kitivo
cha Uchumi cha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Rais Kikwete ameongeza
kuwa,
katika sekta ya elimu licha ya kuwa na changamoto kadhaa, lakini
serikali imepiga hatua kubwa ya maendeleo kutokana na kuongezeka kwa
idadi ya wanafunzi wanaoandikishwa kwenye darasa la kwanza, wanafunzi wa
sekondari na vyuo vikuu na vile vya ufundi. Hata hivyo Rais Kikwete
amekiri kwamba Tanzania inakabiliwa na upungufu wa walimu wa masomo ya
sayansi, na kwamba jambo hilo linapaswa kutafutiwa suluhisho.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment