KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA DIWANI ATHUMANI
Na, Gordon
Kalulunga, Mbeya
JESHI la
polisi mkoani Mbeya limewafikisha mahakamani askari wa Nne wa Jeshi la wananchi
wa Tanzania kwa tuhuma za mauaji.
Taarifa ya
Jeshi la Polisi mkoani Mbeya iliyosainiwa na Kamanda wa polisi wa mkoa huo
Diwani Athumani iliyotumwa kwa vyombo vya habari jana, imesema kuwa mnamo
Novemba 18 huko katika hospitali teule ya wilaya ya Mbeya Vijijini Petro Sanga
(25) alifariki dunia akipatiwa matibabu baada ya kuchomwa kisu.
Kamanda
Diwani Athumani kupitia taarifa hiyo amesema kuwa marehemu alichomwa kisu
shingoni na kikundi cha watu wanaosadikiwa kuwa ni wanajeshi kikosi cha 44 KJ
Mbalizi akiwa kwenye Grocery inayoitwa Vavene Mwe.
‘’Marehemu
baada ya watu hao kuvamia Bar iitwayo Power Night Club na kuwapiga ambamo awali
alikuwepo na kushambuliwa alijaribu kukimbia toka eneo hilo hadi katika Grocery
hiyo lakini watu hao walimkimbiza hadi eneo la hilo na kumjeruhi vibaya kwa
kumchoma kisu.
Amesema
chanzo cha tukio hil ilikuwa ni kulipiza kisasi baada ya askari Godfrey
Matete(30) wa kikosi hicho kupigwa na walinzi wa kilabu cha pombe za kienyeji
kiitwacho DDC kilichopo Mbalizi ambapo
askari huyo alifungua kesi katika kituo cha polsi cha Mbalizi ambapo walinzi
hao wane walikamatwa.
Amewataja
walinzi ambao walikamatwa kuwa ni pamoja na Frenk Mtasimwa (25, Mure
Julius(26), Omary Charles(28) na Legnard Mwampete(30) ambapo baada ya kukamatwa
upelelezi unaendelea.
Amesema
kufuatia utambuzi wa askari hao, askari kumi walikamatwa lakini upelelezi
umebaini kuwa askari wane ndiyo waliohusika na tukio hilo la mauaji hivyo jeshi
la polisi limewafikisha jana katika mahakama ya hakimu mkazi mkoa wa Mbeya na
kusomewa mashitaka na mwanasheria wa SerikaliAchiles Paul Mulisa.
Askari
waliofikishwa mahakamani na kusomewa shitaka hilo ni pamoa na MT 101269 Omary
Mwichande(24), MT 101271 Rajabu Mussa(23), MT 101263 Mussa Vuai Hassan (24) na
MT 99506 Richard Costa Frisch(24) ambapo nwote wamekana shitaka lao na kesi imehairishwa mpaka Desemba 12, mwaka huu.
Kamanda
Diwan Athuman ametoa wito kwa jamii kuepukana na tabia ya kujichukulia sheria
mkononi na pindi wanapotendewa isivyo halali ni vizuri kutoa malalamiko yao
katika mamlaka husika vilevile alisema kuwa ni vema jamii ikajenga tabia ya
kutii sheria bila shuruti.
No comments:
Post a Comment