Waasi nchini Jamhuri ya Afrika ya
Kati wameudhibiti mji wa kaskazini wa Kabo ulioko karibu na mpaka wa
nchi jirani ya Chad. Afisa mmoja wa jeshi la Jamhuri ya Afrika ya Kati
ambaye hakutaka jina lake litajwe amesema waasi hao wa muungano wa
Seleka wamekata mawasiliano yote na mji wa Kabo ambao wanaushikilia hivi
sasa. Shambulio hilo la waasi limefanywa siku moja baada ya vikosi vya
jeshi la Chad kuingia katika ardhi ya Jamhuri ya Afrika ya Kati kuitikia
ombi la serikali ya Bangui la kuisaidia kuzima uasi nchini humo. Wakati
huohuo Umoja wa Afrika umewataka waasi wa Seleka kuondoka katika mji
huo wanaoushikilia huku waasi hao wakisisitiza kusonga mbele kuelekea
kusini mwa nchi hiyo.
Kamanda wa waasi hao Djouma Narkoyo amethibitisha
kwamba wameuteka mji wa Kabo na wanasonga mbele kuelekea mji wa
Batangafo. Waasi wa Jamhuri ya Afrika ya Kati wametishia kumuangusha
Rais wa nchi hiyo Francois Bozize aliyetwaa madaraka mwaka 2003 kupitia
mapinduzi ya kijeshi. Waasi hao wanamtuhumu kiongozi huyo kuwa amekiuka
makubaliano ya amani aliyofikia na makundiu tofauti ya waasi kati ya
mwaka 2007 na 2011…/
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment