Jumla ya asilimia 63.8 ya Wamisri
waliopiga kura katika kura ya maoni ya hivi karibuni nchini humo
wameunga mkono kuidhinishwa rasimu ya katiba mpya ya nchi hiyo. Samir
Abu al Matti Mkuu wa Kamisheni Kuu ya Uchaguzi ya Misri ametangaza
matokeo hayo jana katika mkutano na vyombo vya habari huko Cairo mji
mkuu wa nchi hiyo. Wakati huo huo Hisham Qandil Waziri Mkuu wa Misri
ametoa taarifa akisema kuwa hakuna aliyeshindwa kwenye kura hiyo ya
maoni na kwamba katiba mpya ya Misri itakuwa ya Wamisri wote. Ameyataka
pia makundi yote ya kisiasa kushirikiana na serikali ili kuisaidia nchi
hiyo kufufua uchumi wake.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment