Social Icons

rss feed facebook twitter google plus linkedin youtube email

Sunday, December 30, 2012

Mazoezi ya kijeshi ya "Velayat 91" yaendelea Iran


Mazoezi ya kijeshi ya fukweni angani na baharini ya JKI katika maji ya ghuba ya uajemi ya "Velayat 91" Mazoezi ya kijeshi ya fukweni angani na baharini ya JKI katika maji ya ghuba ya uajemi ya "Velayat 91"
Mazoezi ya kijeshi ya "Velayat 91" yameendelea leo hapa nchini Iran katika siku yake ya tatu.
Maneva hayo ya siku sita yalianza juzi, tarehe 28 Disemba, na yanafanyika katika eneo pana la fukweni, baharini na angani kwenye lango la Hormuz, Bahari ya Oman, kaskazini mwa Bahari ya Hindi, Ghuba ya Aden na lango la Babul Mandab.

Msemaji wa luteka hiyo ya kijeshi, Admeri Amir Rastegari amesema kuwa, leo Timu ya Vita vya Mtandao wa Kompyuta ya jeshi la majini imefanikiwa kugundua tishio katika mtandao huo na kulizuia lisishambulie.
Maneva hayo ya kijeshi ya Iran yana ujumbe wa urafiki na udugu kwa mataifa rafiki na onyo kali kwa maadui.
Katika miaka ya hivi karibuni, Iran imekabiliwa na mashambulio kadhaa ya mtandao wa kompyuta.
"Timu ya Ulinzi wa Mtandao wa Komyuta" inaundwa na wataalamu waliobobea wa Iran na kazi yake ni kulinda mtandao wa kompyuta wa vikosi vya majini vya Iran.

No comments:

Post a Comment