Wizara ya Mawasiliano ya Posta na
Simu ya Lebanon imelikataa ombi la Marekani la kutaka kujenga kituo cha
mawasiliano ndani ya ardhi ya nchi hiyo. Taarifa iliyotolewa na wizara
hiyo imeeleza kuwa hatua hiyo inakinzana na misingi ya kidiplomasia na
inakiuka pia mamlaka ya kujitawala ya Lebanon. Wakati huo huo Faisal
Daud, kiongozi wa harakati ya mapambano ya Kiarabu ya Lebanon amesema,
kutokana na kugunduliwa mitandao kadhaa ya kijasusi ya utawala wa
Kizayuni wa Israel ndani ya ardhi ya Lebanon kujengwa kituo cha
mawasiliano ya posta na simu cha Marekani ndani ya ardhi ya nchi hiyo ni
hatua ya kwanza ya kutumikia na kudhamini maslahi ya utawala wa
kizayuni katika eneo.
Wataalamu wa masuala ya kisiasa na usalama katika
eneo wanalitathmini ombi hilo la Marekani kuwa ni sehemu ya mkakati wa
kijasusi wa Washington dhidi ya muqawama na nchi za eneo la Mashariki ya
Kati hususan Syria, na ni kwa sababu hiyo ombi hilo limekataliwa na
serikali ya Beirut. Hata hivyo wataalamu hao wanaamini kwamba Washington
itaishinikiza zaidi serikali ya Lebanon mpaka ihakikishe inapata kibali
cha kujenga kituo hicho…/
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment