Rais Hamid Karzai wa Afghanistan
amekiri kwamba Shirika la Kijeshi la NATO pamoja na Marekani
zinasababisha nchi hiyo ikose uthabiti. Karzai amesema, sehemu ya
ukosefu usalama nchini kwake inatokana na operesheni za NATO na Marekani
na kuvikosoa vikosi vya kigeni vinavyoongozwa na Marekani kwa
kutekeleza mashambulizi ya usiku na kuua raia wasio na hatia
. Aidha Rais
Karzai ametishia kwamba atasimamisha mazungumzo kuhusiana na hatima ya
vikosi vya Marekani nchini Afghanistan. Wananchi wa Afghanistan wamezidi
kukasirishwa na mauaji ya raia wasio na hatia yanayotekelezwa na vikosi
vya kigeni vikiongozwa na Marekani nchini kwao. Marekani inadai kwamba
inawashambulia wafuasi wa Taliban lakini raia ndio wahanga wakubwa wa
mashambulizi hao.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment