Umoja wa Afrika umeutaka Umoja wa Mataifa ukubali haraka
iwezekanavyo mpango wa kupelekwa kikosi cha kimataifa cha kulinda amani
kaskazini mwa Mali.
Takwa hilo limekabidhiwa rasmi kwa Umoja wa Mataifa na Maraisi Thomas Boni Yayi wa Benin ambaye pia ni Mwenyekiti wa sasa wa Umoja wa Afrika na Idriss Deby wa Chad kwa niaba ya Umoja wa Afrika.
Viongozi hao wa Kiafrika wameeleza kuwa, hatua ya kupelekwa kikosi cha kimataifa cha kulinda amani huko kaskazini mwa Mali, itasaidia kukomesha mgogoro huo. Viongozi hao wameitaka jamii ya kimataifa kufanya juhudi kubwa za kutatua kwa haraka mgogoro wa Mali.
Imepangwa kuwa, Rais Blaise Compaore wa Burkina Faso ambaye ni mpatanishi wa mgogoro huo kutoka Jumuiya ya Uchumi ya Magharibi mwa Afrika ECOWAS leo atakutana na kufanya mazungumzo na vinara wa makundi ya Ansar Diin na National Movement for the Liberation of Azawad (MNLA).
Wakuu wa nchi wanachama wa ECOWAS tarehe 11 Novemba waliafiki kwa pamoja mpango wa kutumwa wanajeshi 3,300 huko kaskazini mwa Mali, kwa shabaha ya kukabiliana na waasi wa eneo hilo.

No comments:
Post a Comment