George Little Msemaji wa Wizara ya
Ulinzi ya Marekani (Pentagon) amekiri kwamba ndege isiyo na rubani
iliyonaswa na Iran baada ya kuingia kinyemela katika anga ya Ghuba ya
Uajemi imetengenezwa Marekani. Hata hivyo Little amedai kwamba kukamatwa
ndege hiyo hakuthibitishi kwamba imetumwa nchini Iran na Marekani.
Matamshi hayo ya msemaji wa Pentagoni
ni ya kwanza kutolewa na maafisa
wa Marekani kuhusiana na ndege yao hiyo isiyo na rubani, suala ambalo
wamekuwa wakilikana tangu habari hiyo ilipotangazwa na Iran. Jumatano
Kamanda wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran (IRGC)
alitangaza kwamba wamefanikiwa kukamata ndege ya kijasusi ya Marekani
isiyo na rubani punde baada ya kuingia katika anga ya Iran kinyume cha
sheria. Aidha Brigedia Jenerali Ramazan Sharif Mkuu wa Idara ya Habari
ya IRGC alitangaza kwamba wamefanikiwa kuchomoa habari na taarifa zote
za siri katika ndege hiyo ya kijasusi isiyo na rubani (drone) ya
Marekani aina ya ScanEagle iliyonaswa hivi karibuni na jeshi la Iran.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment