skip to main |
skip to sidebar
Ehsanoghlo: Hali ya Syria ni nyeti zaidi Ma/ Kati
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Ushirikiano ya Nchi za Kiislamu OIC
amesema kuwa hali ya mambo huko Syria ni nyeti. Ikmaluddin Ehsanoghlo
amesema kuwa Syria iko katika mazingira nyeti zaidi na kwamba katika
mazingira hayo nchi hiyo inapasa kujiepusha na mambo yasiyo na taathira
yoyote katika kufanikisha kufikiwa mwenendo wa uhuru na demokrasia
nchini humo. Katibu Mkuu wa Jumuiya ya OIC kesho Jumatano anatazamia
kuelekea Morocco kwa ajili ya kushiriki kwenye kikao cha "Marafiki wa
Syria." Syria imekuwa ikikabiliwa na hali ya mchafukoge tangu mwezi
Machi mwaka jana, machafuko ambayo hadi sasa yamepelekea kuuawa wananchi
vikiwemo vikosi vya usalama vya nchi hiyo.
No comments:
Post a Comment