Duru za habari kutoka nchini Kodivaa
zinaarifu kuwa, watu wasiojulikana wenye silaha wamekishambulia kituo
cha upekuzi nchini humo na kuwajeruhi askari wawili. Watu walioshuhudia
wamesema kuwa, askari walilazimika kujibu na hivyo kusababisha kuzuka
mapigano kati ya vikosi vya usalama na watu hao wenye silaha. Tangu
mwezi Agost mwaka huu Ivory Coast imekuwa ikishuhudia silsila ya mauaji
ya kuvizia, yanayofanywa na watu wasiojulikana wenye silaha,
dhidi ya
askari wa kulinda usalama na vituo vya kijeshi nchini humo. Serikali ya
Ivory Coast inayahusisha mauaji hayo na askari watiifu kwa aliyekuwa
rais wa nchi hiyo Laurent Gbagbo, ambaye hivi sasa kesi yake inaendelea
kusikilizwa na Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ICC ya mjini Hague,
Uholanzi. Hayo yanajiri katika hali ambayo, jana Mahakama Kuu ya Ivory
Coast ilitangaza kukubaliana na ombi la aliyekuwa Waziri Mkuu wa Gbagbo
Bwana Gilbert Marie Aké N'Gbo pamoja na watu saba wengine waliokuwa
wapambe wa rais huyo, aliyetaka kuachiliwa huru kwa muda na mahakama
hiyo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment