Waasi wa M23 wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wametishia kuwa
watarejea tena katika mji wa Goma wa mashariki mwa nchi hiyo endapo
serikali ya Kinshasa haitoafiki kufanya nao mazungumzo hadi kufikia
Jumatatu ya leo. Bertrand Bisimwa mmoja wa wasemaji wa M23 amesema
kwamba, wanaumia sana kuondoka Goma hasa kutokana na kupoteza watu wao
katika mapigano ya kudhibiti mji huo; lakini kwamba kama kufanya hivyo
kutakuwa ni kutoa zawadi kwa mchakato wa amani wanalikubali hilo.
Ameongeza kuwa, marafiki wa Kongo wamewashauri watoe fursa kwa
mazungumzo; lakini kama mazungumzo hayo hayataanza hadi kufikia mchana
wa leo, basi watarejea tena katika mji wa Goma. Hayo yanaripotiwa katika
hali ambayo, tangu waasi wa M23 waondoke Goma, Rais Joseph Kabila
hajaweka wazi hadi sasa kama serikali yake iko tayari kufanya mazungumzo
na waasi hao.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment