Harakati ya Ukombozi ya Palestina (PLO) imetangaza kuwa
Wapalestina zaidi ya 700 wameuawa huko Syria tangu kuzuka kwa mgogoro
nchini humo zaidi ya miezi 21 iliyopita.
Zacharia al Bahja, afisa wa PLO anayehusika na masuala ya wakimbizi amesema kuwa Wapalestina zaidi ya 700 wameuawa huko Syria tangu kuanza kwa machafuko nchini humo yaliyoyajumuisha pia kambi ya Yarmuk nchini humo. Roketi kadhaa zilivurumishwa jana jioni katika kambi ya wakimbizi wa Kipalestina ya Yarmuk huko kusini mwa Damascus mji mkuu wa Syria, eneo ambalo wiki iliyopita lilishuhudia mapigano makali kati ya vikosi vya jeshi la Syria na wanamgambo wanaofadhiliwa na nchi za kigeni. Syria ilisisitiza jana kuwa wanajeshi wake hawajahusika kwa njia yoyote ile katika machafuko hayo.

No comments:
Post a Comment