Idrissa Doucoure Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Kimataifa ya
Maji na Afya ya Afrika amesema kuwa, watu milioni mia tatu wamekosa maji
salama ya kunywa barani humo. Akihutubia kwenye kongamano la pili la
taasisi hiyo huko Dakkar mji mkuu wa Senegal, Doucoure ameongeza kuwa,
licha ya watu milioni mia tatu kukosa maji salama ya kunywa, wengine
milioni mia tano wanakabiliwa na hali mbaya ya ukosefu wa huduma za
afya. Kongamano hilo la siku mbili linawashirikisha wajumbe 700 wakiwemo
mawaziri kutoka nchi 36 za Kiafrika linafanyika kwa shabaha ya kutafuta
njia za kuwekeza katika sekta za maji na huduma za afya barani Afrika.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment