Picha zilizochukuliwa kutoka katika
mji wa Aleppo huko kaskazini magharibi mwa Syria zinaonyesha wamiliki wa
maduka mjini humo wakiuza bidhaa zao mitaani kufuatia kubomolewa maduka
yao na makundi ya magaidi na waasi wanaopigana dhidi ya serikali ya
Rais Bashar al Assad wa nchi hiyo.
Makundi hayo ya wahalifu wenye silaha
ambao wengi wao ni raia wa kigeni wamebomoa na kuiba bidhaa zilizokuwa
ndani ya maduka hayo. Ripoti zinasema kuwa magaidi hao wanaiba pia ngano
na kuiuza nchini Syria. Septemba 29 mwaka huu moto mkubwa uliharibu
mamia ya maduka katika mji huo mkongwe uliotangazwa na Unesco kuwa ni
eneo la turathi za kimataifa. Moto huo ulizuka wakati kulipozuka
mapigano makali kati ya waasi na vikosi vya serikali.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment