Social Icons

rss feed facebook twitter google plus linkedin youtube email

Monday, December 31, 2012

Serikali ya Syria inaunga mkono mazungumzo


Serikali ya Syria inaunga mkono mazungumzo
Waziri Mkuu wa Syria Wael al Halqi amesema kuwa serikali ya Damascus itakubali mpango wowote utakaobuniwa ili kutatua mgogoro wa nchi hiyo kupitia mazungumzo.
Damascus imesema hayo baada ya Lakhdar Brahimi, mpatanishi wa pamoja wa Umoja wa Mataifa na Jumuiya ya Nchi za Kiarabu katika mgogoro wa Syra kutangaza kwamba, ana mpango wa kuhitimisha mapigano nchini humo. Al Halqi amesema, serikali ya Damascus inaunga mkono mpango wa maridhiano ya kitaifa na itakubali suluhisho lolote la kumaliza mgogoro wa nchi hiyo kwa njia za amani,
mazungumo na kuzuia uingiliaji wa kigeni katika masuala ya Syria.
Wakati hayo yakiripotiwa waasi wa Syria wanaopigana na serikali huku wakifadhiliwa na madola ya kigeni wamelipua bomba la gesi mashariki mwa nchi hiyo.

No comments:

Post a Comment