KESI ya madai ya fidia
iliyofunguliwa na wakazi wa Mbagala, Wilayani Temeke, jijini Dar es
Salaam walioathirika na mabomu mwaka 2009 imehamishiwa Baraza la
Usuluhishi ili kutafuta muafaka kati yao na serikali.
baraza la usululishi ili kufanya mazungumzo baina ya pande hizo mbili yaani serikali na wananchi hao.
Akitoa maamuzi hayo jijini
hivi karibuni, baada ya wakili wa serikali, Mikidadi Rashid, kuwasilisha
ombi la serikali ya kutaka shauri hilo lipelekwe katika Baraza hilo,
Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu, Dk. Fauzi Twaib, alisema Mahakama
inakubaliana na ombi hilo.
Shauri hilo limepangwa kuanza kusikilizwa na kikao cha Baraza hilo la Usuluhishi kuanzia Februari 27, 2013.
Jaji Twaibu alisema pande zote
zimekubali kupeleka kesi hiyo kwenye baraza hilo, hivyo Mahakama
inabariki hatua hiyo kwaza na baada ya majadiliano hayo kushindika
ndipo itaazwa kusikilizwa upya.
Akizungumzia hatua hiyo Katibu
msaidiza wa waathirika hao Alvan Agustino .alisema wameafiki hatua hiyo
ya Mahakama ya kutaka kukaa meza ya usululishi na Serikali na kama
itashindikanika kupata muafaka basi kesi itasikilizwa upya.
Alisema Kesi hiyo namba 181 ya
2011 iliifunguliwa na wakazi hao kutokana na kutoridhishwa na kiwango
cha fidia ambacho walilipwa na serikali baada ya mali zao zikiwemo
nyumba kuathiriwa na mabomu yaliyolika katika kambi ya Mbagala Aprili
2009.
Alisema watu zaidi ya 76
hawakuridhishwa na fidia hiyo ambapo serikali hawakukubali kulipa zaidi
na wakaamua kufungua kesi Mahakama kuu na kuidai serikali sh. bilioni
moja.
No comments:
Post a Comment