Wanajeshi 70 wa serikali ya Sudan na
waasi saba wameuwawa kwenye mapigano makali yaliyojiri kati ya vikosi
vya serikali ya Kharoum na waasi hao katika jimbo la Kordofan Kusini.
Arnu Ngutulu Msemaji wa harakati ya Sudan People's Liberation Movement –
North ( SPLM-N) amesema kuwa, harakati hiyo kwa mara nyingine tena
imeshambulia kwa makombora mji wa Kadugli makao makuu ya jimbo hilo.
Mashuhuda wameeleza kuwa,
idadi kubwa ya wakaazi wa eneo hilo
wamelazimika kuyakimbia makazi yao baada ya kushadidi mashambulizi.
Ngutulu amesema kuwa, shambulio hilo la waasi limefanyika ikiwa kulipa
kisasi cha shambulio la anga lililofanywa na ndege za kivita za jeshi la
serikali ya Khartoum kwenye vijiji vya Kordofan Kusini. Serikali ya
Sudan inaituhumu serikali ya Sudan Kusini kwa kuwapatia hifadhi pamoja
na silaha na zana za kivita waasi walioko kwenye mikoa ya Blue Nile,
Kordofan Kusini na eneo la Darfur.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment