Social Icons

rss feed facebook twitter google plus linkedin youtube email

Thursday, November 15, 2012

Wabunge wapinga kupelekwa jeshi Samburu



Wabunge wapinga kupelekwa jeshi Samburu
Wabunge kadhaa nchini Kenya wamesema kuwa, hatua ya Rais Mwai Kibaki ya kuamuru kupelekwa jeshi katika eneo la Samburu ni kinyume cha sharia na ni ukiukaji wa katiba. Wabunge John Munyes, Josephat Nanok na Ekwe Ethuro wamesema kuwa Rais Kibaki hakuomba ridhaa ya bunge kabla ya kuamuru jeshi kupelekwa Samburu kukabiliana na majangili waliowaua maafisa 40 wa polisi mwanzoni mwa wiki hii. Wabunge hao wamesema tayari agizo hilo la rais limesababisha kuweko kwa hali ya wasiwasi na huenda zoezi la kuwaandikisha wapiga kura linalotarajiwa kuanza wiki ijayo likaathiriwa pakubwa.
Ofisi ya rais haijatoa radiamali yoyote kwa madai ya wabunge hao na habari zinaeleza kuwa tayari wanajeshi wamewasili katika eneo la Baragoi huko Samburu kukabiliana na wezi wa mifugo waliowaua maafisa wa polisi.

No comments:

Post a Comment