Waziri wa Mambo ya Nje wa Misri amesisitizia udharura wa
kutafutwa suluhisho la mwisho la mgogoro wa Palestina. Muhammad Kamal
Amru amesema hayo katika hotuba yake kwenye mkutano wa kwanza kati ya
kundi la Misri na Ulaya mjini Cairo.
Amesisitiza kadhia ya Palestina kutafutiwa suluhisho la mwisho, suala la kwanza likiwa kurejea wakimbizi wa Palestina katika ardhi yao ukiwemo mji wa Quds na katika maeneo ya vitongoji vya walowezi wa Kizayuni.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Misri aidha ametaka kuheshimiwa dini, uhuru wa kutoa maoni na pia kukabiliana na vitendo vya kuvunjia heshima viongozi na dini za mbinguni.
Wakati huo huo Waziri Mkuu wa serikali halali ya Palestina amesema, viongozi wa Misri walioingia madarakani baada ya mapinduzi ya wananchi wanapinga mashambulizi mapya dhidi ya Gaza.
Haniya ameongeza kuwa, iwapo Israel isingeungwa mkono na Marekani na nchi za Kiarabu na kama nchi hizo zisingenyamazia kimya jinai za utawala huo huko Ghaza, basi Tel Aviv isingethubutu kuushambulia ukanda huo.

No comments:
Post a Comment