Social Icons

rss feed facebook twitter google plus linkedin youtube email

Thursday, November 29, 2012

Mapambano ya polisi na waandamanaji Cairo


Mapambano ya polisi na waandamanaji CairoMapambano baina ya waandamanaji Misri na polisi yameendelea leo mjini Cairo kwa siku ya sita mfululizo kwa lengo la kupinga hatua ya Rais Mohammad Mursi kujiongozea madaraka.
Wafanya maandamano wanataka kufutwa amri iliyotangazwa wiki iliyopita na Rais Mursi wa nchi hiyo ambayo inamzidishia uwezo wake wa kimadaraka.
Wamisri sasa wamemtaka Rais Muhammad Mursi wa nchi hiyo ajiuzulu hiyo ikiwa ni katika kuendelea kulalamikia utendaji wa rais huyo.
Wiki iliyopita, Rais Mursi alitoa dikrii inayopiga marufuku kuvunjwa baraza la katiba lililopewa jukumu kisheria la kutunga katiba mpya ya nchi hiyo. Aidha Mursi amemfuta kazi mwendesha mashtaka mkuu kutokana na kufanya uzembe katika kesi inayomkabili dikteta wa zamani wa nchi hiyo Hosni Mubarak. Mursi ametetea maamuzi aliyochukua akisisitiza kwamba amefanya hivyo ili kuyalinda mapinduzi ya wananchi na kuongeza kuwa juhudi zake zinalenga kurejesha mamlaka na uhuru wa mihimili mitatu mikuu ya dola, yaani Serikali, Bunge na Mahakama.

No comments:

Post a Comment