Duru za habari zimeeleza kuwa, viongozi wa Saudi Arabia wamefanya
kikao cha siri mjini Riyadh kwa shabaha ya kuyaongezea nguvu zaidi
makundi ya waasi wanaobeba silaha dhidi ya serikali ya Syria. Toleo la
leo la gazeti la al Quds al Arabi limeandika kuwa, viongozi wa Saudi
Arabia na nchi nyingine za Kiarabu wamefanya kikao cha siri na kufikia
natija ya kutoa mafunzo zaidi ya kijeshi kwa waasi wa Syria kwa lengo la
kutekeleza operesheni zaidi za kigaidi nchini humo. Taarifa zinaeleza
kuwa, kwenye kikao hicho imekubaliwa kwamba kundi la waasi wapatao elfu
tatu lipelekwe katika eneo la Tabuk nchini Saudi Arabia kwa shabaha ya
kupata mafunzo zaidi ya kijeshi na kutekeleza operesheni za kigaidi
katika mikoa ya Idlib na Halab iliyoko kaskazini magharibi mwa Syria.
Taarifa hizo zimeeleza kuwa, mafunzo hayo kwa magaidi, yatatolewa na
maafisa wastaafu wa jeshi la Saudi Arabia yamelenga kuharibu miundombinu
ya Syria.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment