skip to main |
skip to sidebar
Wafuasi wa Rais Mursi waandamana hadi ikulu
Mamia ya raia wa Misri wanaoumuunga mkono Rais Muhammad Mursi wa
nchi hiyo leo wameandamana hadi katika ikulu ya rais wa nchi hiyo na
kutangaza kuunga mkono uamuzi wake wa kumfukuza kazi mwendesha mashtaka
mkuu na kuzuia kuvunjwa baraza la kutunga katiba la nchi hiyo. Mamia ya
Wamisri wanaomuunga mkono Rais Muhammad Mursi mapema leo wameandamana
huku wakipiga nara za kumuunga mkono rais wao katika maamuzi
aliyochukua hapo jana ya kutangaza mabadiliko ya katiba ili kupanua
uwezo wake. Rais wa Misri jana alitoa taarifa ya kisheria na kueleza
kuwa hakuna chombo chochote cha kisheria kinachoweza kulivunja baraza la
kutunga katiba la nchi hiyo. Mabadiliko hayo ya kisheria yanasisitiza
kuhukumiwa upya Hosni Mubarak dikteta aliyeng'olewa madarakani huko
Misri pamoja na viongozi wa zama za utawala wake wanaotuhumiwa kuwauwa
wanamapinduzi na kufanya ufisadi katika uga wa kisiasa nchini humo.
No comments:
Post a Comment