Serikali ya China imetoa msaada wa 
karibu euro milioni kumi kwa Umoja wa Afrika kwa shabaha ya kusaidia 
operesheni za vikosi vya kulinda amani barani humo. Makubaliano hayo 
yametiwa saini kati ya serikali ya China na Umoja wa Afrika yenye lengo 
la kudhamini gharama za maandalizi ya operesheni za kulinda amani barani
 humo. Erastus Mwencha Msaidizi wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika amesema 
kuwa, msaada huo wa China utasaidia katika utekelezwaji wa operesheni ya
 umoja huo nchini Somalia, nchi ambayo kwa kiasi fulani imeshaanza 
kupata utulifu. Inafaa kuashiria hapa kuwa, mwezi Novemba mwaka 2011, 
China ilikabidhi jengo jipya la Umoja wa Afrika nchini Ethiopia, makao 
makuu ya umoja huo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)







 

 
 
 
 
 





 
 







No comments:
Post a Comment