Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Issa Bin Shaaban Simba amelaaani
jinai za utawala wa Kizayuni wa Israel huko Gaza Palestina ambapo makumi
ya wanawake, watoto, wazee na vijana wasio na hatia wameuawa hivi
karibuni kufuatia hujuma na amshambulio ya Israel dhidi ya Ukanda wa
Gaza. Mufti Simba amesema, analaani mauaji yanayofanywa na Israel dhidi
ya wananchi wa Palestina. Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari,
Mufti Mkuu wa Tanzania amesema, anatoa wito kwa viongozi wa kitaifa na
wale wa kimataifa, likiwemo Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa wa
kutafuta haraka suluhisho la kudumu la kadhia ya Palestina. Amesema,
Baraza Kuu la Waislamu nchini Tanzania BAKWATA siku zote limekuwa na
itaendelea kuwa mstari wa mbele kuunga mkono harakati za Wapalestina za
kupigania haki zao za kimsingi ikiwemo ya kuwa na nchi yao huru ya
Palestina.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment