Social Icons

rss feed facebook twitter google plus linkedin youtube email

Sunday, November 18, 2012

UN yalaani mashambulizi ya M23 mashariki mwa DRC



UN yalaani mashambulizi ya M23 mashariki mwa DRC
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa  limelaani vikali mashambulizi ya waasi wa M23 mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo kwenye maeneo ya Kibumba, Mboga na Ruhondo, pamoja na kuendelea kuukaribia mji wa Goma.
Katika kikao cha Jumamosi mjini New York, Baraza la Usalama pia limewataka waasi hao kuheshimu majukumu ya vikosi vya usalama vya Umoja wa Mataifa, MONUSCO. Baraza la Usalama pia limetoa wito kwa nchi zilizo na ushawishi kwa waasi wa M23 yawashawishi waasi hao wakomeshe mashambulizi. Wataalamu wa Umoja wa Mataifa wanasema Uganda na Rwanda zinaunga mkono waasi hao wa M23. Kikao hicho cha Baraza la Usalama kiliitishwa kufuatia ombi la serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo, kutokana na hali ya usalama inayoendelea kuzorota. Baraza la Usalama limesema kamati namba 1533 itaundwa, ambayo itapokea mapendekezo ya mataifa wanachama, na baadaye hatua zitachukuliwa kulingana na mapendekezo hayo.

No comments:

Post a Comment