Mahakama za Tanzania zimeendelea
kuwashikilia jela viongozi kadhaa wa Kiislamu nchini humo. Huko visiwani
Zanzibar, Amiri wa Jumuiya ya Maimamu Zanzibar Sheikh Farid Hadi na
masheikh wengine kadhaa akiwemo Sheikh Mselem Ali Mselem na Sheikh Azan
Khalid Hamdan wa Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu JUMIKI
wameendelea kubakia rumande baada ya kuwekewa masharti mazito ya
dhamana. Huku hayo yakiripotiwa, mawakili wa viongozi hao wa taasisi za
Kiislamu Zanzibar wamelalamika vikali kuwa wateja wao wanavunjiwa haki
ikiwa ni pamoja na kunyolewa ndevu bila ya ridhaa zao wakiwa rumande.
Hati ya mkurugenzi wa mashtaka Zanzibar ndiyo iliyotumika kuendelea
kuwaweka rumande masheikh hao. Vile vile jana Alkhamisi mkurugenzi wa
mashtaka Tanzania Bara (DPP) aliendelea kumuweka rumande Katibu wa
Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Shekhe Ponda Issa Ponda.
Miongoni mwa mashtaka yanayowakabili viongozi hao wa taasisi za Kiislamu
Tanzania ni uchochezi na kusababisha fujo na uvunjifu wa amani. Taarifa
nyingine zinasema kuwa Waislamu 49 wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu
Tanzania wameachiliwa huru kwa dhamana.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment