Jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo limewashmbulia waasi wa kundi la M23 na kuwaua raia 10.
Msemaji wa M23 Betran Bisimwa ametoa madai hayo na kuongeza kuwa watu hao wameuawa wakati vikosi vya serikali viliposhambulia ngome ya waasi katika eneo la Kitagoma mashariki mwa Kongo karibu na mpaka wa Uganda. Amesema shambulizi hilo lilijiri Ijumaa na kwamba waasi walifanikiwa kuwarudisha nyuma wanajeshi wa serikali. Hatahivyo Jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo limekanusha kutekeleza shambulizi hilo na kusema eneo la Kitagoma liko mikononi mwa waasi wa M23. Msemaji wa Jeshi la Kongo katika mkowa wa Kivu Kaskazini Kanali Oliveir Hamuli amesema waasi wa M23 ndio waliowaua raia hao na wanajaribu kuvilaumu vikosi vya serikali.
Aghalabu ya wapiganaji katika kundi la M23 walikimbia jeshi la Kongo mwezi Aprili mwaka huu kwa madai kuwa serikali ya Kinshasa imeshindwa kutekeleza makubalianao ya amani yaliyotiwa saini Machi 2009. Waasi hao wanashikilia eneo ndogo katika mkoa wa Kivu Kaskazini karibu na mji wa Goma.

No comments:
Post a Comment