Askari wawili wa kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa
katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo MONUSCO wamejeruhiwa baada ya
kujiri mapigano na waasi wa kundi la M23 katika eneo la mashariki mwa
nchi hiyo.
Taarifa zinasema kuwa, mapigano hayo yametokea katika eneo la Pinga lililopo katika jimbo la Kivu Kaskazini na kusababisha kifo cha askari mmoja wa jeshi la Kongo na kujeruhi idadi kadhaa ya wananchi katika eneo hilo. Mapigano katika eneo hilo kati ya vikosi vya serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na waasi wa M23 yanaendelea kwa miezi kadhaa sasa na yamewalazimisha watu wasiopungua laki tatu kuyakimbia makazi yao.
Hivi karibuni wataalamu wa Umoja wa Mataifa walitoa ripoti inayosisitiza kuwa nchi za Rwanda na Uganda zinawaunga mkono waasi hao, tuhuma ambazo zimekadhibishwa vikali na serikali za Kampala na Kigali.

No comments:
Post a Comment